Jumapili 10 Mei 2026 - 19:30
Dunia imeingia katika mfumo mpya baada ya Vita vya Ramadhani / Tumefikia hatua ya kuamua mambo baada ya kuwa katika hatua ya kujihami

Hawza/ Hujjatul Islam wal-Muslimin Hussein Kouhsari, akisisitiza kwamba; hawza ndio mstari wa mbele wa medani ya mapambano dhidi ya mfumo wa ubeberu, alisema: Dunia imeingia katika mfumo mpya baada ya Vita vya Ramadhani, na tumefikia hatua ya kuamua mambo baada ya kuwa katika hatua ya kujihami.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul Islam wal-Muslimin Sayyid Mufid Hussein Kouhsari, katika kikao cha pili cha ubainishaji kilichokuwa na mada isemayo; “Iran na Vita vya Tatu vya Kulazimishwa; kwa mtazamo wa wanazuoni na viongozi wa dini na madhehebu”, ambacho kiliandaliwa na Taasisi ya Sheikh Ansari mjini Qom Iran, huku akirejelea kumbukumbu ya mwaka ya kutolewa kwa “Hati ya Hawza Inayoongoza na Bora”, alifafanua vipengele vyake vya kimataifa. Na huku akisisitiza kwamba; hati hiyo ni zaidi ya waraka wa kitaifa, alisema: Hati ya “Hawza Inayoongoza na Bora” ni hati yenye sura ya kimataifa na ya ustaarabu wa dunia nzima. Kipengele cha kimataifa katika hati hii si suala moja pembeni mwa maelfu ya masuala mengine, bali ni roho inayotawala vipengele vyake vyote.

Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza, huku akirejelea vipengele vitano vinavyojenga utambulisho wa hawza kwa mujibu wa mtazamo wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi, alisema: Katika vipengele hivi vitano, vipengele viwili vina sura ya wazi kabisa ya kimataifa:


Kwanza, hawza ndiyo mstari wa mbele wa kukabiliana na mfumo wa ubeberu na mfumo dhalimu;

Pili, hawza inayoongoza na bora ni hawza ya kimataifa na yenye kujenga ustaarabu. Yaani sehemu mbili kati ya tano za nguzo zinazojenga utambulisho wa hawza zimeundwa kwa mtazamo wa kimataifa, na hata katika pande tatu nyingine roho ya kimataifa imepenyezwa kikamilifu.

Hujjatul Islam wal-Muslimin Hussein Kouhsari, huku akisema kwamba hawza za kielimu si taasisi za elimu pekee, alisisitiza: Hawza ndiyo mstari wa mbele wa medani ya mapambano dhidi ya mfumo wa ubeberu.

Aliongeza kiwa: Katika fikra za Kiongozi Shahidi, mfumo wa ubeberu ni mfumo wa fikra wenye masharti manne ya kuporomoka kwake (kuondoka Marekani katika eneo, mwisho wa utawala wa Kizayuni, mwisho wa mfumo wa kibeberu katika medani ya kimataifa, na kudhoofika kwa ustaarabu wa Magharibi), ambapo Vita vya Kulazimishwa vya Ramadhani vimeleta mabadiliko ya kimkakati katika mihimili yote minne.

Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza, akitoa uchambuzi wa kimkakati kuhusu mabadiliko baada ya “Vita vya Ramadhani” na athari zake, alisema: Dunia ya kabla ya vita hivi ni tofauti kabisa na dunia ya baada yake, na sasa tunashuhudia kuzaliwa kwa mfumo mpya wa kimataifa, Ghuba mpya ya Uajemi, Muqawama mpya, na hata Ulaya na Marekani mpya.

Kuporomoka kwa mfumo wa zamani na kudhoofika kwa tawala ya Marekani

Hujjatul Islam wal-Muslimin Kouhsari alisema: Umbali kati ya kabla na baada ya Vita vya Ramadhani ni mkubwa zaidi kuliko miezi miwili. Leo tunashuhudia kuthibitishwa kwa kushindwa kwa taasisi kama Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama.

Aliongeza kiwa: Tupo katika kipindi nyeti cha kihistoria ambapo Marekani imeanza kutoka katika uwepo wa moja kwa moja na tawala ya kibabe kuelekea kwenye kujiondoa kwa udhibiti maalumu na pia mgogoro wa uhalali wake.

Mwalimu wa Hawza ya Qom, huku akirejelea kushindwa kwa miundo ya kimataifa, alisema: Utawala wa Kizayuni umetoka katika simulizi ya “ubora wa moja kwa moja” na kauli mbiu ya “kutoka Nile hadi Furati” na kufikia mgogoro wa uwepo na uchakavu wa kimkakati usioweza kurekebishwa. Na pia uchawi wa uwezo wa kijeshi wa Marekani wa kuzuia umevunjika milele katika vita hivi.

Mabadiliko katika eneo na Muqawama; kutoka kuzuia hadi kuamua mambo

Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza nchini Iran, akirejelea kubadilika kwa mizania katika eneo la Ghuba ya Uajemi, alisema: Eneo la Ghuba ya Uajemi limevuka utegemezi kamili wa kisiasa na kiusalama kwa Marekani na kuingia katika mizania yenye akili. Mafanikio muhimu zaidi ni kupita kwa Muqawama kutoka katika hatua ya “kuzuia” hadi hatua ya “kuamua mambo” katika eneo.

Hujjatul Islam wal-Muslimin Hussein Kouhsari alielezea mabadiliko muhimu zaidi kuwa ni haya yafuatayo:

Umoja wa kioperesheni usio na mfano kati ya mihimili ya Muqawama.

Kupita kutoka vita vya kujihami kwenda vita vya mashambulizi na vita mseto vya kijeshi, kiuchumi, kiutambuzi na vya kimedia.

Kubadilika kwa fikra ya Muqawama kuwa mfano unaotoa hamasa katika kiwango cha kimataifa. Changamoto ya kiteolojia kwa Uwahabi na Ukristo wa Kizayuni; tetemeko kubwa zaidi la kiitikadi

Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza za Kiislamu, kuhusiana na athari za kiitikadi na kifalsafa za Vita vya Kulazimishwa vya Ramadhani, alisema: Vita hivi vimeleta athari kubwa zaidi za kiteolojia kwa mkondo wa Uwahabi.

Alifafanua: Katika vitabu vya Mawahabi mara nyingi iliandikwa kwamba; Mashia kamwe hawataingia katika vita vya moja kwa moja na Wayahudi, lakini Vita vya Ramadhani na majibu ya Muqawama vimevunja uchawi huo. Leo wanazuoni wengi wa Ahlus-Sunnah wanatangaza waziwazi kwamba: “Kwa maisha yetu yote tulikuwa tunafikiri kimakosa.”

Hujjatul Islam wal-Muslimin Husseini Kouhsari pia alirejelea changamoto ya makundi ya Wakristo wa Kizayuni (Evangelists) na kusema: Wanaamini kwamba kwa ajili ya kudhihiri kwa Nabii Issa (as), lazima dola yenye nguvu ya Kiyahudi iundwe katika Yerusalemu; lakini leo wanaona kwamba kinyume na imani yao, utawala wa Kizayuni uko katika hali ya kuporomoka, na hili ni tetemeko kubwa la kiitikadi kwao.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha